Trending News>>

Tume ya Utumishi wa walimu nchini yalaani tukio la mwanafunzi kupigwa mkoani Mbeya.

Siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa za walimu kumuadhibu kinyama mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya kutwa ya Mbeya Tume ya Utumishi wa walimu nchini imelaani tukio hilo na kuitaka serikali iwachukulie hatua kali wahusika kwa kuwa kanuni za adhabu kwa wanafunzi ambazo pamoja na mambo mengine zinaagiza kuwepo kwa kibali kutoka kwa mwalimu mkuu.

Walimu hao ambao walikuwa kwenye mafunzo kivitendo wakitokea Chuo kikuu cha Dar es Salaam na chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere walimuadhibu mwanafunzi Sebastian Chinguku na kisha picha za tukio hilo kusambaa kwenye mitandao hali iliyoibua mihemuko kwa jamii na kusababisha baadhi ya viongozi wa juu wa serikali kutoa matamko ikiwemo kuagizwa walimu hao wakamatwe .

Aidha Bi Winifrida Rutainurwa Katibu Tume ya walimu nchni amefafanua kanuni za adhabu kwa wanafunzi ambapo miongoni mwake ni ile inayowataka walimu wanafunzi na walimu waliopo kazini kutoa adhabu kwa wanafunzi kwa ruhusa au kibali kutoka kwa mwalimu mkuu.

No comments:

Powered by Blogger.