NHC yambwaga Mbowe mahakamani
Mwekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameangukia pua mahakamani baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutupilia mbali maombi yake katika mgogoro wake wa umiliki wa jengo la Shirika la Nyumba (NHC).
Mbowe alifungua maombi mahakamani hapo kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd, akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo ambalo alikuwa akilitumia kama ofisi ya kampuni yake ya Magazeti ya Free Media na klab ya Bilicanas.
Katika maombi hayo, pamoja na mambo mengine Mbowe alikuwa akidai kuwa aliondolewa katika jengo hilo jinyume cha sheria kwa kuwa hakupewa taarifa na kwamba kampuni ya udalali iliyotumiwa kumuondoa haijasajiliwa kama dalali wa mahakama.
Hata hivyo katika uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, imetupilia mbali maombi hayo ya Mbowe ikisema kuwa hayana msingi
Jaji Mwangesi alikubaliana na hoja za NHC na akasema kuwa Mbowe aliondolewa katika jengo hilo kisheria.
No comments:
Post a Comment