Trending News>>

Liverpool kuvaa jezi maalum leo ikiwa ni kampeni ya kuzuia upofu


Kuelekea mchezo wa leo kati ya Man United na Liverpool watavaa jezi maalum zilizoandikwa “Seeing is Believing” (Kuona ni kuamini) ikiwa ni kutoa sapoti ya kuongeza uelewa wa kampeni ya kuzuia upofu na uharibifu wa uwezo wa kuona.

Liverpool wataungana na wadhamini wao Standard Chartered wanafanya hivyo zikiwa zimepita siku 4 tangu kuazimishwa kwa “World Sight Day” ambayo huazimishwa kila mwaka kwa lengo la kuleta ufahamu juu ya upofu na uharibifu wa uwezo wa kuona.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ” nikiwa kama mtu ninayevaa miwani ,ninafahamu kuona ni muhimu katika maisha yangu .kwa hiyo hili suala ni muhimu sana kwangu.”

Miwani ya Klopp itapigwa mnada baada ya mchezo ili kuchangia pesa katika kampeni hiyo, na jezi za wachezaji za mechi hiyo, pamoja na kitambaa cha unahodha pia vitauzwa kwa ajili ya kuongeza fedha za kusaidia kampeni hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.