Kisa Tuzo, Mashabiki ‘Wamfunda’ Harmonize
Sikia hii! Baada ya mkali wa Bongo Fleva nchini anayetamba na Ngoma ya Matatizo, Harmonize kushinda Tuzo ya Afrimma (African Muzik Magazine Awards), iliyofanyikia Dallas, Marekani katika kipengele cha Msanii Bora Chipukizi, Afrika Mashariki mashabiki wa kazi zake wamemtaka kukaza buti huku wakimchana ‘live’ kuwa akilegea kidogo tu msanii mwenzake kutoka kwenye lebo yao ya Wasafi Classic, Ray Vanny atamfunika.
Mashabiki hao walimfunda msanii huyo kupitia kwenye mitandao ya kijamii lakini pia walimpongeza kwa ushindi huo na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Wengine walioshinda kutoka Tanzania ni pamoja na Diamond Platnumz aliyechukua Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki na DJ D- Ommy aliyechukua Tuzo ya DJ Bora wa Afrika
No comments:
Post a Comment