Unakumbuka magoli ya ajabu ambayo aliyekuwa nyota wa zamani wa Arsenal alitimka Emirate 2012 na kumfuata Ferguson baadae akachukua ubingwa wa England kwa mara ya kwanza, huyu ni Robin Van Persie huwa anafunga magoli ya ajabu ajabu sana haswa pale anapopata nafasi.
Unakumbuka lile goli ambalo alipata pasi kutoka nyuma ya eneo la katikati ya uwanja kutoka kwa Wayne Rooney ? Ilikuwa kati ya Manchester United dhidi ya Aston Villa ile pasi ikaja nyuma yake ikampita akaiunganisha na kuingia nyavuni moja kwa moja, sio mara ya kwanza kufunga magoli kama yale aliwahi kufunga goli lile 2005 kati ya Arsenal na Leeds United pasi ikatoka kwa Emanuel Eboue upande wa kulia akapiga mua kama alioupiga akiwa Manchester United na kuweka kimiani.
Sasa goli lake limechaguliwa kuwa goli bora kule EPL tukio hilo limefanyika katika jiji la London kutimiza miaka 25 ya Ligi Kuu England, mchakato ulikuwa mkubwa maana walichaguliwa wachezaji mbalimbali ambao waliowahi kufunga magoli 100 na zaidi katika ligi hiyo na goli lake ndilo likachaguliwa goli bora.
Baada ya hafla hiyo Van Persie amechangia watoto wenye mazingira magumu kiasi cha £20,000 kwa ajili ya watoto hao, katika maelezo yake Persie amesema amefurahi sana kwa tukio hilo na anajihisi furaha sana hasa ukizingatia ndio ubingwa wake wa kwanza akicheza nchi hiyo.
GOLI LA VAN PERSIE LAWA GOLI BORA EPL
Reviewed by
Unknown
on
October 09, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment