Diamond Aanza Mazoezi ya Kuimba Live na Band Kama Ali Kiba...Show za Uingereza na Neyo Atazipiga na Band

Diamond Platnumz anatarajia kufanya ‘tour’ ya muziki nchini Uingereza akiwa na mwanamuziki Ne-Yo siku za karibuni. Lakini pia alisema kuwa maandalizi ya kuimba na bendi sio tu kwa ajili ya ‘tour’ hiyo kwani hata kwenye matamasha mengine atakuwa akiimba ‘live’.

Aidha, alieleza kuwa alichelewa kuanza kutumia bendi kwa sababu alikuwa akitaka apate wapigaji vyombo wenye ujuzi. Unajua wakati mwingine unaweza ukawa unaimba na bendi lakini ukaonekana unaimba vibaya sababu ya upigaji mbaya wa vyombo, mimi sikutaka hilo ndio sababu ilinichukua muda ili nipate watu wazuri, alisema Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment