Trending News>>

Dawa ya asili ya ugonjwa wa moyo


Ugonjwa wa moyo  unajumuisha matatizo ambayo yanaathiri muundo na kazi za MOYO. Ugonjwa wa moyo mara nyingi huhusishwa na kujibana au kukazika kwa mishipa ya damu, au mkusanyiko wa taka katika kuta za mishipa ya damu ambako hupelekea kupungua kipenyo cha mishipa ya damu na hivyo kuzuia mzunguko ulio huru wa damu, na hatimaye kukupa hatari ya kupata shambulio la moyo na stroke.

Ugonjwa wa moyo unahusisha matatizo kama matatizo ya mishipa ya moyo, matatizo ya kurithi ya moyo, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, moyo kufeli kufanya kazi, matatizo ya valve za moyo, moyo mpana au mkubwa na matatizo mengine mengi katika moyo.

 Chanzo na dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine kutegemea na aina ya ugonjwa wa moyo. Baadhi ya dalili za kawaida ni pamoja na pumzi fupi, maumivu ya kifua, mapigo ya chini ya moyo, kichwa kizito, uchovu na udhaifu wa mwili kwa ujumla.

Vitu vingine vinavyoweza kuongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo ni pamoja na:

a)Shinikizo la juu la damu
b)Kolesto
c)Kisukari
d)Uzito kupita kiasi
e)Uvutaji sigara
f)Unywaji pombe kupita kiasi
g)Matumizi yaliyozidi ya kaffeina
h)Utumiaji wa madawa ya kulevya
i)Uzee
j)Kutokujishughulisha na mazoezi
j)Kurithi
k)Mfadhaiko wa akili (stress)

Wakati unataka kujitibu ugonjwa wa moyo ni mhimu kutofanya lolote wewe mwenyewe peke yako bila ushauri au uangalizi wa karibu wa daktari au muuguzi wako. Unaweza pia kutumia baadhi ya dawa za asili na kubadili namna unavyoishi ili kuimarisha afya ya moyo wako.

Baadhi ya hizi dawa za asili zinaweza zisipatane na baadhi ya dawa za hospitalini kama upo unatumia dozi ya ugonjwa fulani wakati huu. Kwahiyo pata ushauri kwanza toka kwa mtaalamu wa afya aliye karibu na unayemwamini kabla hujaamua kutumia baadhi ya hizi dawa.

1. Mafuta ya Habbat Soda
Moyo usio na afya unaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi sana lakini chanzo kikuu cha sababu zote hizo ni kimoja, nacho ni kutokuupa moyo virutubishi mhimu unavyovihitaji kila siku ili ubaki na afya.

Mafuta ya asili ya Habbat Soda yana kiinilishe mhimu sana kwa afya ya moyo ambacho ni asidi amino Omega 6 na 9 na kiilishe kingine kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘phytosterols’. Viinilishe hivi mhimu husaidia kuzuia mishipa kujikaza na hivyo kuwa msaada mkubwa hata kwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Viinilishe hivi kwenye mafuta asili ya habbat soda husaidia kushusha kolesto na sukari katika damu pia.

Kwa karne nyingi mafuta ya asili ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu ugonjwa moyo.
Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chakula cha mafuta haya kutwa mara 2 kwa majuma hata miezi kadhaa. Unaweza kuchanganya mafuta haya kwenye glasi moja ya juisi yoyote uliyotengeneza nyumbani ili kuupata radha.

2. Kitunguu Swaumu
Tafiti kadhaa zimeonyesha kitunguu swaumu kuwa na ufanisi mkubwa sana katika kutibu magonjwa kama shinikizo la juu la damu, kolesteroli na magonjwa ya mishipa ya moyo. Kitunguu swaumu huzuia kujikaza au kuzibika kwa mishipa ya damu. Kitunguu swaumu pia huongeza msukumo wa damu. Ili kujitibu au kujizuia usipate ugonjwa wa moyo kwa kitunguu swaumu fanya hivi;

Kula punje moja au mbili za kitunguu swaumu kila siku. Ikiwa inakutokea radha yake au harufu yake inakuwa kali sana unaweza kunywa glasi moja ya maziwa freshi baada ya kuwa umekula hizo punje za kitunguu swaumu.
 Mhimu: Kitunguu swaumu kinaweza kisipatane na aina nyingi ya dawa za hospitalini sababu ya baadhi ya dawa hizo hukaza mishipa ya damu. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza kutumia hii dawa.

3. Bizari (manjano)
Tafiti zinaonyesha kwamba bizari inao uwezo wa kuzuia mishipa ya damu kujikaza. Bizari inayo kirutubishi mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘curcumin’ ambacho husaidia kutunza afya ya moyo kwa kuzipunguza taka taka za kolesto, takataka nyingine zozote kwenye mishipa ya damu na kuzuia kuganda kwa damu kwa ujumla.

Bizari pia inasaidia kushusha msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto ((LDL) na kuzuia uundwaji wa uvimbe. Inao uwezo mkubwa pia wa kuondoa sumu mwilini na hivyo kuzuia kujijenga kwa vijidudu nyemelezi vya magonjwa (free radicals) na kama matokeo yake ya pili husaidia kutozeeka mapema na magonjwa mengine sugu.

Tumia bizari mara nyingi au kama kiungo kwenye vyakula vingi unavyopika.
Unaweza pia kuchemsha kijiko kikubwa kimoja cha chakula na maji nusu  lita au na maziwa nusu lita (vikombe viwili). Kunywa  kikombe kimoja asubuhi na kikombe kingine jioni  kila siku kwa wiki kadhaa.

4. Uwatu
Uwatu una sifa kuu ya kuondoa sumu mwilini na kuulinda mfumo mzima wa upumuaji. Uwatu husaidia kupunguza uwezekano wa ateri za damu kuzibika (atherosclerosis), hurekebisha na kuweka sawa usawa wa mafuta katika damu (blood lipid).

Uwatu pia husaidia seli damu za damu kutokuumana na kukaribiana sifa ambayo ni mhimu sana katika kuzuia damu kuganda na hivyo kupunguza hatari kugandana au kushikana kwa seli za damu kusiko kwa kawaida kunakohusiana na shambulio la moyo, kushusha kolesto, sukari katika damu na mafuta yaliyozidi.


  • Loweka kijiko kidogo kimoja (kijiko cha chai) cha mbegu za uwatu kwa usiku mzima.
  • Siku inayofuata kula hizo mbegu za uwatu zilizokuwa zimeloweka wakati tumbo likiwa tupu.
  • Fanya hivyo kila siku kwa miezi kadhaa.

5. Chai ya kijani (Green Tea)
Chai ya kijani maarufu kama ‘Green tea’ ina viondoa sumu vya mhimu sana mwilini ambavyo husaidia kuimarisha afya ya seli zinazounda sehemu ya ndani kabisa za moyo na mishipa ya damu. Husaidia kushusha kolesto na kiwango cha mafuta katika damu. Chai hii pia husaidia kudhibiti sukari katika damu (blood sugar) na kuimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Katika utafiti uliofanywa na Japani mwaka 2008, watafiti waligundua kuwa kunywa vikombe vitano vya chai hii ya kijani kwa siku kulisaidia kupunguza hatari ya kupatwa na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa moyo au stroke kwa asilimia 26.

Kunywa vikombe vinne kila siku vya chai hii ya kijani (kumbuka usiongeze ndani yake yale majani mengine meusi ya chai ili kuepuka kaffeina).

6. Mazoezi
Utanishangaa mazoezi nayo ni dawa? Ndiyo mazoezi ni dawa tena ni dawa kwa magonjwa mengi sana mwilini tofauti na unavyodhani. Tatizo watu wengi hawajishughulishi na mazoezi labda mpaka waambiwe au washauriwe na daktari. Mazoezi ni mhimu kwa mtu yeyote uwe unaumwa au huumwi chochote.

Mazoezi ya mara kwa mara yakiambatana na kula lishe sahihi inaweza kusaidia kuzuia na kuudhibiti ugonjwa wa moyo. Mazoezi kama ya kutembea  kwa miguu, kukimbia pole pole (jogging), kuendesha baiskeli  na kuruka kamba ni mazoezi ya mhimu sana katika kuuongezea nguvu moyo wako na mfumo wa upumuaji, kuimarisha mzunguko wa damu na kushusha shinikizo la juu la damu.

Mazoezi husaidia pia kudhiti uzito na unene kupita kiasi wa mwili na hivyo kupunguza msongo wa mawazo (stress) vitu ambavyo vina uhusiano wa karibu kati ya ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine mengi.

Chama cha madaktari wa magonjwa ya moyo cha Marekani kinashauri kila mtu kufanya mazoezi ya walau nusu saa kila siku mara tano kwa wiki ili kuimarisha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Ongea na daktari juu ya mazoezi gani yanakufaa kwa mjibu wa uzito wako.

7. Magnesium na Potassium
Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kutumia madini ya magnesium kunaweza kupunguza shinikizo la juu la damu na kwamba ni madini mazuri kwa ufanyaji kazi wa jumla wa moyo.

Utafiti mwingine umeonyesha utumiaji wa potassium unasaidia kuboresha kazi za moyo vile vile husaidia kupunguza shinikizo la juu la damu kutokana na utumiaji uliozidi wa chumvi.

Unaweza kuwa umeshaambiwa kuwa utumiaji wa chumvi ya mezani (sodium chloride) ni jambo baya, lakini kwa kutumia chumvi yenye magnesium na potassium badala ya chumvi ya mezani kunaweza kusaidia sana kushusha shinikizo la juu la damu kama inavyoelezwa kwenye utafiti huu.

Mambo ya mhimu kuzingatia:

  • Punguza mafuta, kolesto na chumvi kwenye chakula chako.
  • Epuka mafuta magumu hasa yale yatokanayo na wanyama (polyunsaturated and monounsaturated fats). Mfano unaweza kutumia mafuta ya zeituni badala ya kutumia siagi, margarine na mafuta mengine yatokanayo na wanyama.
  • Acha kuvuta sigara na punguza kunywa pombe
  • Punguza uzito, hakikisha una uzito kulingana na urefu wako.
  • Punguzo mawazo (stress) na tumia mbinu mbadala za ku-relax (kupumzika).
  • Epuka ugonjwa wa kisukari.
  • Pata vitu vyenye omega 3 na vitamin D
  • Pata usingizi wa kutosha kila siku.
  • Fanya vipimo vya jumla juu ya afya yako kila mara.

Je Umeipenda makala hii? Ninakaribisha mchango wako wa mawazo au ikiwa una swali nitafurahi zaidi kwani ni faraja kwangu kuona nimekujibu vizuri.

No comments:

Powered by Blogger.