CHAMA cha Wananchi (CUF) wilayani hapa kimetoa tamko la kutomtambua
Mwenyekiti wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, na kwamba hakitampokea
katika ziara yake.
Lipumba anatarajia kuanza ziara mkoani Tanga kesho huku uongozi wa
chama hicho ukisisitiza kutambua uamuzi wa Mkutano Mkuu uliomwondoa
madarakani na wa Baraza Kuu kumvua uanachama.
Mwenyekiti wa CUF wa Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe alitoa tamko hilo
jana akieleza kuwa hawatakuwa tayari kukaidi Katiba ya Chama chao na
kwamba hawatampokea na hakuna maandalizi yatakayofanyika kumpokea.
"Tumeambiwa Lipumba ana dhamira ya kufanya ziara mkoani hapa. Sisi kwa
uamuzi wa Baraza hatumtambui, wala hatujaandaa maandalizi ya kumpokea.
“Wilaya za Korogwe na Muheza ndizo zimesema atazitembelea, lakini sisi
hatuko pamoja nao na watakaompokea wataingia kwenye mgogoro mwingine kwa
sababu hatambuliki," alisema Jumbe.
Mwenyekiti huyo pia alizungumzia mgogoro baina yao na CCM kutokana na
sakata la umeya ambapo alisema hatima ya mgogoro huo itajulikana baada
ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.
Alisema kutokana na sakata hilo walitoa malalamiko kwa viongozi
mbalimbali lakini hakuna hatua zozote zinazoendelea, hivyo Kamati ya
Utendaji iliwataka madiwani wa chama hicho kutohudhuria kikao chochote
cha Halmashauri hadi itakapotoa uamuzi.
"Tumetoa malalamiko yetu kwa viongozi wa CCMna lengo letu ilikuwa
tuonane na Rais lakini tulimpata Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
aliyetwambia kuwa atalifanyia kazi, lakini sasa tumeamua kupeleka
malalamiko yetu kwa wenye chama na wao ndio watakaotoa uamuzi juu ya
mgogoro huo.
“Hivyo tumeitisha mkutano ambao utakuwa na wajumbe 440 ambapo tuna imani kuwa tatizo letu litakwisha Oktoba 29,” alisema Jumbe.
CUF Tanga Wamgomea Profesa Lipumba
Reviewed by
Unknown
on
October 13, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment