Beki aliyempiga Neymar agoma kuomba msamaha
Beki wa Bolivia, Yasmani Duk anayetuhumiwa kumpiga kiwiko nahodha wa Brazil, Neymar, amegoma kuomba msamaha.
Duk amesema kamwe hawezi kufanya hivyo kwa kuwa hakuna kosa alilofanya.
Beki huyo mwenye mwili wa kimazoezi hasa, amesisitiza alimgonga Neymar kwa bahati mbaya lakini suala hilo linakuzwa.
Hivyo Duk, amezidi kuweka msisitizo kwamba hataomba radii hata kidogo.
Picha za mechi kati ya Brazil dhidi ya Bolivia zinaonyesha Duk alimgonga Neymar na asilimia kubwa ilikuwa ni bahati mbaya.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya kuwania kucheza Kombe la Dunia kwa nchi za Amerika Kusini.
No comments:
Post a Comment